Waziri wa Mambo ya Ndani Uingereza: Wahajiri wanakimbia ubaguzi nchini Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62864-waziri_wa_mambo_ya_ndani_uingereza_wahajiri_wanakimbia_ubaguzi_nchini_ufaransa
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza amesema kuwa wahajiri wanaingia Uingereza wakitokea Ufaransa wakisema Ufaransa ni nchi ya kibaguzi.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 17, 2020 03:48 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Ndani Uingereza: Wahajiri wanakimbia ubaguzi nchini Ufaransa

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza amesema kuwa wahajiri wanaingia Uingereza wakitokea Ufaransa wakisema Ufaransa ni nchi ya kibaguzi.

Priti Patel ameliambia Bunge la Uingereza kwamba, wahajiri wanaingia nchini wakisema Ufaransa ni nchi ya kibaguzi na kwamba mtazamo huo si wake yeye bali wa wahajiri. 

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza amesema hayo baada ya kuongezeka idadi ya watu wanaohama Ufaransa na kuelekea Uingereza kwa kutumia mitumbwi.

Hadi sasa Ufaransa haijatoa tamko lolote kuhusu kadhia hiyo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza imetangaza kuwa, waziri Priti Patel amekasirishwa na idadi kubwa na inayoongezeka kila siku ya wahajiri wanaotoka Ufarasa na kuingia nchini humo. 

Maafisa wa serikali ya Uingereza wamekuwa wakilalamikia idadi ya kubwa ya wahajiri wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria wakitokea Ufaransa kupitia mfereji wa English Channel. 

Wanaharakati wa kutetea haki za wahajiri pia wanalalamikia mienendo mibaya uinayowakabiliwa wahajiri katika nchi za Ulaya ikiwemo Ufaransa na Uingereza.