Ajali mbaya ya treni yaua na kujeruhi watu 108 nchini Taiwan
Watu 108 wameuawa na kujeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea mashariki ya kisiwa cha Taiwan
Idara ya usafiri na uchukuzi ya Taiwan imetangaza kuwa, ajali hiyo imetokea leo asubuhi kwa saa za nchi hiyo wakati treni ya abiria ilipogongana na lori na kusababisha treni hiyo kuacha njia.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, watu wasiopungua 54 wamefariki na wengine 72 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kisiwa cha Taiwan katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.
Shirika rasmi la habari la Taiwan limetangaza kuwa, lori lililogongana na treni halikuwa limeegeshwa vizuri na kuna uwezekano lilikuwa kwenye iliyopita treni hiyo na hivyo kusababisha ajali.

Kwa mujibu wa Idara ya Zimamoto, treni iliyopata ajali ilikuwa ikitoka mji mkuu Taipei kuelekea Taitung wakati ilipoanja njia katika njia ya chini ya ardhi iliyopo kaskazini ya eneo la Hualien na kusababisha mabehewa kadhaa kugongana na kuta za njia hiyo.
Waziri wa usafiri na uchukuzi wa Taiwan Lin Chia-lung amewaeleza waandishi wa habari kuwa treni hiyo ilikuwa na abiria 490, na akaongeza kwamba, majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa hospitali baada ya shughuli ya uokozi iliyofanyika katika mazingira magumu ya kupenya kwenye njia ya chini ya ardhi katika eneo la ajali.../