Assad: Syria inaiunga mkono Russia katika kukabiliana na uhasama wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i69504-assad_syria_inaiunga_mkono_russia_katika_kukabiliana_na_uhasama_wa_magharibi
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema nchi yake inaunga mkono jitihada za Russia za kukabiliana na chokochoko na hatua za uhasama za baadhi ya nchi za Magharibi na nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO zikiongozwa na Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 27, 2021 08:31 UTC
  • Assad: Syria inaiunga mkono Russia katika kukabiliana na uhasama wa Magharibi

Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema nchi yake inaunga mkono jitihada za Russia za kukabiliana na chokochoko na hatua za uhasama za baadhi ya nchi za Magharibi na nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO zikiongozwa na Marekani.

Rais Assad amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin na kuongeza kuwa, "Syria inaunga mkono juhudi za Russia za kukabiliana na uchokozi wa Wamagharibi hususan katika eneo la mashariki mwa Ukraine.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limemnukuu Rais Bashar al-Assad akisema kuwa, hatua za Wamagharibi zinalenga kudunisha nafasi ya Russia na sera zake athirifu ambazo msingi wake ni kutaka kuwepo uelewa wa sheria za kimataifa na kupatikana uthabiti katika maeneo yote ya dunia.

Rais wa Syria amesema nchi za Magharibi zinafanya juu chini kushadidisha hali ya taharuki duniani, hususan katika mzozo unaoihusu Ukraine.

Taharuki baina ya Russia na Ukraine inayochochewa na Wamagharibi

Russia na nchi za Magharibi zimekuwa katika mkwaruzano kwa miaka mingi juu ya eneo la mashariki mwa Ukraine ambalo wakazi wake wanazungumza Kirusi.

Eneo hilo limeshuhudia makabiliano ya umwagaji damu tokea mwaka 2014, baina ya vikosi vya serikali ya Kiev na vile vya Russia.