Makaburi ya Waislamu Ufaransa yabomolewa na makundi yenye misimamo mikali
Chuki dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa zinazidi kuongezeka baada ya makaburi ya Waislamu kushambuliwa na makundi yenye misimamo ya kufurutu mpaka.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Mulhouse ulioko mashariki mwa Ufaransa ambapo makumi ya makaburi ya Waislamu yamebolewa.
Meya wa mji huo ameziambia duru za habari kwamba, katu hawawezi kuvumiliai vitendo kama hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Taarifa zinasema kwamba, watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa fikra za kufurutu ada na ambao wana chuki na Uislamu wameyashambulia makaburi ya Waislamu katika mji huo wa mashariki mwa nchi hiyo ya bara Ulaya.
Tayari polisi ya mji huo wa Mulhouse imeanzisha uchunguzi wa kitendo hicho ambacho si mara ya kwanza kufanyika nchini Ufaransa.
Mwezi uliopita pia misikiti mitatu nchiini Ufaransa ilivunjiwa heshima kaktika miji ya Montlebon, Pontarlier na Roubaix baada ya kuandikwa katika kuta za misikio hiyo maneno ya chuki dhidi ya Uislamu na Uislamu.
Wafuasi wa makundi na vyama vya kufurutu ada nchini Ufaransa ni miongoni mwa wafuasi wa mrengo wenye misimamo ya utaifa ambao kikawaida ndio ambao huhusika na vitendo kama hivi. Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waisalamu nchini Ufaransa vimeongezeka mno katika siku.
Waislamu nchini Ufaransa wamejitokeza mara kadhaa na kueleza wasiwasi wao kwa vitendo cha hujuma na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) hususan hujuma dhidi ya misikiti na vituo vya Kiislamu.