Apr 02, 2022 02:35 UTC
  • Mashambulizi dhidi ya askari wa US yameongezeka kwa 400% tangu auawe Soleimani

Washington imekiri kuwa, tangu Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) auawe kigaidi nchini Iraq, mashambulizi dhidi ya askari wa Marekani yameongezeka kwa asilimia 400.

Ned Price, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema kati ya mwaka 2019 na 2020, hujuma za makundi yanayofungamana na Iran nchini Iraq dhidi ya wanajeshi wa US  ziliongezeka kwa asilimia 400.

Aidha amesema kitu kingine kilichopelekea kuongezeka mashambulizi dhidi ya vikosi vya Marekani katika eneo la Asia Magharibi ni hatua ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump kuiondoa nchini hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mwaka 2018, na kuanzisha kampeni kubwa ya mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Jenerali Soleimani aliuawa kidhulma uraiani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, tena akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq mnamo Januari 3 mwaka 2020, kwa amri ya Trump.

Shambulizi la askari magaidi wa US dhidi ya gari lililokuwa limembeba Shahidi Soleimani na wanajihadi wenzake

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameeleza kuwa, hatua ya nchi hiyo kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika orodha yake ya makundi ya kigaidi imechangia pia kushtadi hujuma dhidi ya askari wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Ned Price amesisitiza kuwa, sera zote za utawala uliopita wa Marekani dhidi ya Iran zilifeli na kugonga mwamba, na matokeo yake yamekuwa kinyume kabisa na matarajio ya Washington.

Tags