Sep 22, 2022 02:08 UTC
  • Indhari ya FAO: Watu karibu milioni moja wanakabiliwa na hatari ya njaa

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetahadharisha kuwa watu karibu milioni moja wanakabiliwa na hatari ya kukumbwa na njaa katika maeneo mbalimbali duniani.

Shirika la FAO limetoa indhari hiyo ambapo mwaka huu wa 2022 watu karibu milioni moja huko Afghanistan, Ethiopia, Sudan Kusini, Somalia na Yemen wanapoteza maisha kwa kukosa misaada ya chakula na kuongezeka uhaba wa chakula duniani. 

Ripoti ya FAO inaeleza kuwa, ukame mkali ulioathiri eneo la Pembe ya Afrika umepelekea raia katika baadhi ya maeneo ya Ukanda huo kukumbwa na njaa. Aidha ukosefu wa usalama wa chakula unazidi kuongezeka kwa kasi duniani ambapo hali ya mambo huwenda ikawa mbaya zaidi katika miezi ijayo iwapo misaada ya dharura ya kibinadamu haitatolewa. 

Ukame  na baa la njaa;natja ya mabadiliko ya tabia nchi

Mapigano na athari za mabadiliko ya tabianchi ni sababu kuu za kushuhudiwa njaa kali katika maeneo mbalimbali duniani; ambapo mwaka huu wa 2022 hali hii imechochewa pakubwa na kuyumba hali ya uchumi kulikosababishwa na janga la Corona na vita vya Ukraine. 

Tags