May 31, 2023 09:58 UTC
  • Noam Chomsky
    Noam Chomsky

Mwanafalsafa na mwanaisimu mashuhuri wa Marekani ameonya kuhusu matokeo mabaya ya Ulaya kuwa chini ya udhibiti wa Marekani.

Noam Chomsky ameonya katika mahojiano yake na Sputnik yaliyochapishwa leo, kwamba ikiwa Ulaya inataka kuendelea kuwa chini ya udhibiti wa Marekani, kuna uwezekano kwamba itaporomoka na kuondolewa katika safu ya kundi la nchi zilizoendelea kiviwanda.

Mapema Mei 2023, mwekezaji wa Marekani, Jim Rogers, aliiambia Sputnik kwamba jumuiya za kisiasa kama Umoja wa Ulaya, kamwe hazijawahi kudumu katika historia, na jumuiya hiyo kwa sasa inazongwa na matatizo mengi.

Jim Rogers

Marekani daima imekuwa ikidai kuwa kiongozi wa ulimwengu wa kambi moja, na imefanikiwa kuiburuta Ulaya katika njia hiyo.

Mabadiliko ya hali ya kisiasa na kiuchumi duniani, hasa katika miongo ya hivi karibuni, pamoja na kuongezeka kwa nguvu za kiuchumi na kisiasa za China, Russia na baadhi ya nchi duniani, kumewafanya maafisa wa nchi za Magharibi kuwa na wasiwasi juu ya kufikia tamati kipindi cha udhibiti wa Magharibi na ulimwengu wa kambi moja.

Tags