-
Hania: Mashahidi wa Palestina wamethibitisha kuwa Quds ni mstari mwekundu
May 22, 2021 02:08Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amegusia jinsi Wapalestina walivyouliwa shahidi na Wazayuni katika vita vya Quds na kusisitiza kuwa, mashahidi hao wamewathibitisha watu wote kwamba Quds na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa taifa hilo na umma wote wa Kiislamu.
-
Maelfu ya Wapalestina washiriki katika Sala ya Idul Fitr kwenye Msikiti wa al Aqsa
May 13, 2021 07:07Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr leo Alkhamisi asubuhi katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni ambao siku chache zilizopita wanajeshi wa utawala huo katili waliwashambulia kwa mabomu Waislamu waliokuwa wanasali ndani ya Msikiti huo.
-
Wapalestina wa Quds wawashukuru wenzao wa Ghaza kwa kuwapiga wanajeshi Wazayuni kwa makombora
May 11, 2021 03:12Wapalestina wa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni wamefanya maandamano ya kutangaza kufurahishwa kwao na Wapalestina wenzao wa Ghaza kwa kuguswa na hali yao na kujibu jinai za Wazayuni huko Quds kwa kushambulia kwa makombora maeneo ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni.
-
Hamas: Kuichezea Quds ni moto utakaowachoma viongozi wa Israel
May 10, 2021 06:37Naibu Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unacheza na moto kwa kuendelea kuhujumu Baitul Muqaddas na kibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Wanachama wa Harakati ya Kiislamu Nigeria washiriki matembezi ya Siku ya Quds
May 08, 2021 07:51Wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria jana Ijumaa walijitokeza kwa wingi katika matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika miji mikubwa ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Iran yalaani hujuma ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa
May 08, 2021 03:17Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali hujuma ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa wakati Wapalestina walipokuwa katika eneo hilo takatifu kwa ajili ya ibada.
-
Kurejea Wapalestina katika ardhi zao ndio suluhu ya kadhia ya Palestina
May 07, 2021 03:51Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu limesema kutimuliwa Wazayuni maghasibu na kurejea Wapalestina katika ardhi za mababu zao ndilo suluhisho pekee la mgogoro wa Palestina-Israel.
-
Hizbullah: Ukombozi wa Quds umekaribia zaidi ya wakati wowote ule
May 06, 2021 08:15Mkuu wa Baraza Kuu la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema ukombozi wa Quds tukufu umejongea wakati huu, kuliko wakati mwingine wowote ule.
-
Abdollahian: Iran ina stratejia maalumu ya kuwaunga mkono Wapalestina
May 05, 2021 03:02Mshauri maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema Iran ina stratejia maalumu, thabiti na kabambe ya kuwaunga mkono na kuwasaidia wananchi wa Palestina.
-
Mataifa ya Kiislamu yatakiwa kulipa uzito suala la ukombozi wa Quds
May 05, 2021 02:00Mwanaharakati mmoja nchini Russia ametoa mwito kwa mataifa ya Kiislamu kulipa kipaumbele cha kwanza suala la ukombozi wa Quds tukufu na kadhia ya Palestina kwa ujumla.