Dec 31, 2020 07:36 UTC
  • Sheikh Naim Qassim: kuuliwa kigaidi shahid Suleimani kumedhihirisha kilele cha udhaifu wa Marekani katika eneo

Sheikh Naim Qassim amesema kuwa Marekani imemuuwa kigaidi Luteni jenerali Haji Qassem Suleimani nchini Iraq kutokana na kuwa dhaifu.

Akizungumza katika mahojiano na "You News" , Sheikh Naim Qassem Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa kumuuwa kigaidi Luteni Jenerali Suleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) lilikuwa pia lengo la utawala wa Kizayuni.  

Shahid Qassem Suleimani  

Ameongeza kuwa sisi tutatekeleza jukumu letu kwa njia inayofaa mkabala na mauaji hayo ya kigaidi ya shahid Suleimani. Naibu wa Sayyid Hassan Nasrullah ameendelea kusema kuwa, Luteni Jenerali Suleimani tangu awali alikuwa akipigania kuimarika muqawama katika eneo; na aliunga mkono muqawama wa Kiislamu huko Lebanon dhidi ya utawala wa Kizayuni. 

Luteni Jenerali Haji Qassem Suleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) na Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa Kikosi cha al Hashdu al Sha'abi cha Iraq pamoja na wanajihadi wenzao 8 waliuliwa shahidi alfajiri ya Januari 3 mwaka huu katika barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq kwa amri ya Rais Donald Trump wa Marekani. Mauaji hayo yalifanywa na jeshi la kigaidi la Marekani. 

Tags