Jun 01, 2021 10:35 UTC
  • Utawala wa Kizayuni unazuia kuingizwa misaada ya kibinadamu huko Ghaza

Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni ametishia kushadidisha zaidi mashambulizi huko Ukanda wa Ghaza iwapo eti muqawama utaendeleza mashambulizi yake na kueleza kuwa, kuingizwa misaada ya aina yoyote huko Ghaza kunategemea na kurejeshwa miili ya wanajeshi waliouliwa wa Israel katika eneo hilo.

Licha ya taasisi mbalimbali za kimataifa na jumuiya za kutetea haki za binadamu kusisitiza juu ya ulazima wa kupelekwa haraka iwezekanavyo misaada ya kibinadamu huko Ghaza  kwa ajili ya kulijenga upya eneo hilo, utawala unaouwa watoto wa Kizayuni ungali unazuia kutekelezwa suala hilo.  

Ben Gantz, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena ameshurutisha suala la kuingizwa misaada ya kibindamu huko Ghaza kwa ajili ya wananchi wa Palestina na kurejeshwa miili ya wanajeshi wa utawala huo waliouawa katika eneo hilo na Waisraeli waliotiwa nguvuni na makundi ya muqawama. 

Maafa ya vita vya siku 21 vya Gaza dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza

Gantz aidha amekiri kuwa hasara na maafa yaliyosababishwa kwa Israel na makundi ya muqawama katika vita vya siku 12 ni moja ya kumi tu ya uharibifu ambao Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon inaweza kuusababishia utawala huo. Amesisitiza kuwa, vita vitakuwa vigumu zaidi kwa sababu Hizbullah ina makombora laki moja ambayo baadhi yake yanapiga masafa marefu na mengine yakilenga kwa umakini mkubwa mno maeneo yaliyokusudiwa. 

Huko nyuma pia Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu za Kizayuni alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Intelijinsia ya Misri na kuitaka Cairo iisaidie Tel Aviv kurejesha miili ya wanajeshi wa utawala huo waliouawa huko Ghaza na pia eti Misri isaidie kuidhoofisha harakati ya Hamas ya Palestina. 

Tags