UN yataka kuharakishwa kupokonywa silaha wanamgambo CAR
Umoja wa Mataifa umetaka kupokonywa silaha haraka iwezekanavyo makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Zeid Ra'ad al Hussein Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuna udharura wa kupokonywa silaha wanamgambo wanaobeba silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa iliyotolewa na Zaid Ra'ad imeongeza kuwa japokuwa mwaka huu wa 2016 umeanza vizuri ihuko Jamhuri ya Afrika ya Kati kukiwa na matukio kama kufanyika kwa amani uchaguzi nchini, lakini kujiri matukio tofauti katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kama katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, kunatia wasiwasi. Amesema hatua ya kuwapokonya silaha mapema wanamgambo huko Jamhuri ya Afrika ni jambo lenye udharura kwa kuzingatia hali ya mambo ya sasa nchini humo. Itakumbukwa kuwa Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati katikati ya mwezi Juni mwaka huu ulikumbwa na hujuma na machafuko kutoka kwa makundi yanayobeba silaha.