Mbunge Uganda ataka katiba ibadilishwe ili Museveni aendelee kutawala
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i10834-mbunge_uganda_ataka_katiba_ibadilishwe_ili_museveni_aendelee_kutawala
Kuna uwezekano Rais Yoweri Museveni wa Uganda akaendelea kutawala hata baada ya muhula wake kumalizika kisheria baada mbunge mmoja kupendekeza katiba ibadilishwe ili kuondoa kizingiti cha umri ambacho kinamzuia Museveni kugombea tena urais.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2016 09:03 UTC
  • Mbunge Uganda ataka katiba ibadilishwe ili Museveni aendelee kutawala

Kuna uwezekano Rais Yoweri Museveni wa Uganda akaendelea kutawala hata baada ya muhula wake kumalizika kisheria baada mbunge mmoja kupendekeza katiba ibadilishwe ili kuondoa kizingiti cha umri ambacho kinamzuia Museveni kugombea tena urais.

Mbunge Ann Maria Nankabirwa wa chama tawala cha NRM amelimabia Shirika la Habari la Reuters kuwa atawasilisha pendekezo kwa maafisa wa ngazi za juu chamani ili kuanzishwa mchakato wa kuondoa kizingiti cha umri ili Museveni aweze kugombea urais kwa muhula mwingine.

Katiba ya Uganda inasema mtu yeyote mwenye umri wa zaidi ya miaka 75 hapaswi kugombea kiti cha urais. Museveni ambaye sasa ana umri wa miaka 71 hataweza kutetea kiti chake mwaka 2021 kutokana na kizingiti hicho cha umri.

Iwapo katiba itabadilishwa Museveni ambaye aliingia Madarakani mwaka 1986 ataweza kutawala nchi hiyo kwa miaka 40.

Nankabirwa anasema atawasilisha pendekezo hilo katika kipindi cha wiki moja katika ili mchakato wa kubadilisha katiba uanze.

Museveni alipata ushindi wa asilimia 60 katika uchaguzi wa rais uliofanyika Februari mwaka huu huku mpinzani wake wa karibu Kizza Besigye wa chama chaFDC akipata asilimia 35 ya kura. Wapinzani wanadai uchaguzi huo ulikumbwa na wizi wa kura, vitisho vya maafisa wa usalama na kuhongwa wapiga kura.