Jeshi la Somalia na Amisom zimebuni stratejia mpya dhidi ya al Shabab
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12808-jeshi_la_somalia_na_amisom_zimebuni_stratejia_mpya_dhidi_ya_al_shabab
Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na jeshi la nchi hiyo wamebuni stratejia mpya ya kupambana na kundi la wanamgambo wa al Shabab.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Aug 07, 2016 08:51 UTC
  • Jeshi la Somalia na Amisom zimebuni stratejia mpya dhidi ya al Shabab

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na jeshi la nchi hiyo wamebuni stratejia mpya ya kupambana na kundi la wanamgambo wa al Shabab.

Kamanda wa jeshi la Somalia na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini humo wameafikiana kuhusu stratejia mpya ambayo inapasa kutekelezwa ili kuliangamiza kundi la wanamgambo wa al Shabab, hata hivyo hakuna maelezo ya ziada yaliyotolewa katika uwanja huo.

Wanamgambo wa al Shabab ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya umwagaji damu huko Somalia na pia nje ya nchi hiyo

Maafisa wa jeshi la Somalia wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) walitoa taarifa yao ya pamoja mwishoni mwa kikao cha siku tano kilichofanyika Mogadishu kuhusu suala hilo iliyosisitiza juu ya udharura wa kuzidishwa uungaji mkono wa kijeshi na wa kiraia kwa jeshi la taifa la Somalia na vile vile kuzidishwa mawasiliano kati ya vikosi vya jeshi na kikosi cha AMISOM nchini humo.

Maafisa wa kijeshi wa Somalia na wawakilishi wa Umoja wa Afrika walisisitiza katika kikao hicho juu ya udharura wa kuimarisha uwezo wa jeshi la Somalia ili kulifanya kuwa la kisasa na la kitaalamu na kuongeza kuwa, jeshi hilo linapasa kuwa na uwezo na suhula zinazohitajika ili kudhamini usalama wa nchi baada ya kumalizika muda wa kuhudumu kikosi cha AMISOM nchini humo.

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (AMISOM) wakipiga doria huko Somalia