Sep 23, 2016 14:22 UTC
  • Jeshi la Nigeria lauwa Boko Haram 15 jimboni Borno

Msemaji wa Jeshi la Nigeria ameripoti kuwa wanamgambo 15 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa na jeshi katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi.

Kanali Sani Kukasheka Usman amesema leo kuwa wanamgambo wa Boko Haram walivishambulia vikosi vya jeshi lao wakati walipokuwa wakitekeleza oparesheni ya kuwafurusha wanamgambo hao katika kijiji kimoja karibu na jimbo ola Borno huko kaskazini mashariki mwa Nigeria.

wanamgambo wa Boko Haram wa nchini Nigeria

Msemaji wa Jeshi la Nigeria ameongeza kubainisha kuwa, wanajeshi wao wanne wamejeruhiwa kwenye mapigano hayo na wengine wawili pia wameuawa.  Boko Haram imekuwa ikiyatumia maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria kama makao yao. Katika miezi kadhaa iliyopita serikali ya Nigeria imetekeleza oparesheni kadhaa za kijeshi kwa minajili ya kuondoa tishio la ugaidi lililopo.

Tags