Rais wa Senegal asisitiza kutokomezwa ugaidi barani Afrika
Rais Macky Sall wa Senegal amesisitizia ulazima wa kung'olewa na kutokomezwa mizizi ya ugaidi katika nchi zote za Afrika.
Rais wa Senegal ametoa sisitizo hilo katika hotuba yake mbele ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Amani na Usalama linalofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Dakar.
Sall amesema makundi ya kigaidi ni hatari kubwa kwa nchi za Afrika na akasisitizia ulazima wa kuyatokomeza makundi hayo katika nchi zote za bara hilo kwa kutegemea umoja ndani ya Afrika na majeshi ya eneo hilo.
Rais wa Senegal ametoa sisitizo hilo katika hotuba mbele ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Amani na Usalama la Dakar katika hali ambayo wataalamu wa siasa za Afrika wanaitakidi kuwa kuenea na kushamiri makundi ya kigaidi barani Afrika imekuwa moja ya changamoto muhimu zinazolikabili bara hilo.
Wakati huohuo Kamishna mwandamizi wa Usalama na Amani wa Umoja wa Afrika, Smail Chergui amesisitiza kuhusu ulazima wa kupambana vikali na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram ili kuhakikisha kundi hilo linaangamizwa kikamilifu.
Balozi Chergui ametoa wito huo katika kikao na makamanda waandamizi wa vikosi vya mataifa kadhaa ya bara la Afrika. Amesema ujumbe unaojumuisha maafisa waandamizi wa majeshi ya mataifa kadhaa ya Afrika na mkuu wa ofisi ya AU nchini Chad umeanza kazi ya kuchunguza kwa umakini jinsi ya kuendesha operesheni kali za mashambulio dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram.../