Wanawake Waislamu Nigeria walaani kukandamizwa hijabu
(last modified Thu, 02 Feb 2017 14:01:46 GMT )
Feb 02, 2017 14:01 UTC
  • Wanawake Waislamu Nigeria walaani kukandamizwa hijabu

Muungano wa makundi ya wanawake kwa jina la "Hijab Rights Advocacy Initiative" wa nchini Nigeria jana ulilaani kile ulichokitaja kuwa kuendelea kukandamizwa wanawake wanaovaa vazi la stara la hijabu, na kulitaka bunge la nchi hiyo kubuni sheria ili kukomesha unyanyasaji huo wa wanawake wanaovaa hijabu.

Ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hijabu hapo jana, Muungano huo pia umetaka kuhesabiwa kesi zote za unyanyasaji wa wanawake wenye hijabu kuwa ni udhalilishaji dhidi ya wanawake.

Wanawake Waislamu wa Nigeria katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hijabu 

Muungano huo wa makundi ya wanawake wa Nigeria yanayozijumuisha  taasisi kama vile za za Al- Muminat, The Criterion, Mulism Society of Nigeria, MSSN, Federation of Muslim Women Association of Nigeria na nyingine kadhaa zimeitaka serikali kutoa adhabu kali kwa maafisa wake wanaowadhalilisha wanawake wanaovaa hijabu. Mratibu wa muungano huo Bi Hajia Mutiat Orolu-Balogun alisema jana katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hijabu kuwa, kuvaa vazi la stara la hijabu ni haki yao ya kikatiba ambayo inapaswa kulindwa na serikali kupitia sheria. Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hijabu yalifanyika katika nchi mbalimbali hapo jana.

 

Tags