Radiamali ya serikali ya Somalia kwa mapatano ya Imarati na Somaliland
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25166-radiamali_ya_serikali_ya_somalia_kwa_mapatano_ya_imarati_na_somaliland
Serikali ya Somalia imepinga makubaliano yaliyofikiwa kati ya Jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kwa ajili ya kujenga kambi ya kijeshi ya Abu-Dhabi katika eneo hilo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Feb 15, 2017 03:59 UTC
  • Radiamali ya serikali ya Somalia kwa mapatano ya Imarati na  Somaliland

Serikali ya Somalia imepinga makubaliano yaliyofikiwa kati ya Jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kwa ajili ya kujenga kambi ya kijeshi ya Abu-Dhabi katika eneo hilo.

Nour Farah Mkaguzi wa serikali ya Somalia huko Mogadishu amelaani hatua ya bunge la Jamhuri iliyojitangazia uhuru wake ya Somaliland ya kuafiki mpango wa Imarati wa kutaka kujenga kambi ya kijeshi katika mji wa Berbera na kuitahadharisha Abu-dhabi kuwa Somalia itaifungulia mashtaka umoja huo wa falme za Kiarabu kwa kukiuka sheria za kimataifa.

Jamhuri ya Somaliland iliyojitenga na Somalia

Nour Farah amekutaja kujengwa kambi ya kijeshi ya Imarati katika mji wa Berbera huko katika pwani ya Ghuba ya Aden kuwa ni hatua ya upande mmoja na kuongeza kuwa serikali ya Somalia inajiandaa kuwasilisha mashtaka rasmi dhidi ya Imarati. Wakati huo huo Ahmad Mohammed Silanyo Rais wa Jamhuri ya Somaliland amesema kuwa yeye aliafiki mpango huo wa Imarati ili kutoa ajira katika eneo hilo.  Mpango huo wa Imarati wa kutaka kujenga kambi yake ya kijeshi huko Somaliland umepingwa na nchi jirani zikiwemo Ethiopia na Djibouti. Jamhuri ya Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 na kisha kuutangaza mji wa Hargeisa kuwa mji  mkuu wake.