Wanajeshi wa Sudan waachiliwa huru kwa upatanishi wa Rais Museveni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25960-wanajeshi_wa_sudan_waachiliwa_huru_kwa_upatanishi_wa_rais_museveni
Waasi wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Sudan wamewaachilia huru wanajeshi kadhaa wa nchi hiyo waliokuwa wanawashikilia mateka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 05, 2017 04:09 UTC
  • Wanajeshi wa Sudan waachiliwa huru kwa upatanishi wa Rais Museveni

Waasi wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Sudan wamewaachilia huru wanajeshi kadhaa wa nchi hiyo waliokuwa wanawashikilia mateka.

Shirika la habari la Fars limewanukuu waasi hao wakisema katika taarifa yao kuwa wameamua kuwaachilia huru wanajeshi wote 130 wa serikali ya Sudan waliokuwa wamewateka.

Taarifa ya waasi hao imesema kuwa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametoa mchango mkubwa katika kuachiliwa huru wanajeshi hao kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Wanajeshi wa Sudan

Sheikh Abdullah Arzaq Tiba ambaye ni mmoja wa maulamaa wa Kisufi pamoja na wakuu wa kundi la Saihun wamesaidia kuachiliwa huru mateka waliokuwa wanashikiliwa na waasi huko Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile.

Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Sudan ilianza kuwaachilia huru wanajeshi wa serikali ya Sudan tangu mwaka 2014.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda

 

Tangu mwezi Juni 2011, harakati hiyo imekuwa ikipambana na serikali ya Sudan katika majimbo mawili ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

Harakati hiyo ilikuwa na nafasi kubwa katika kujitenga Sudan Kusini mwaka 2011 kupitia kura ya maoni iliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa.