UN: Imarati imekiuka vikwazo vya silaha, Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30286-un_imarati_imekiuka_vikwazo_vya_silaha_libya
Umoja wa Mataifa umesema kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umekiuka vikwazo vya silaha vya Libya.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 10, 2017 15:56 UTC
  • UN: Imarati imekiuka vikwazo vya silaha, Libya

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umekiuka vikwazo vya silaha vya Libya.

Ripoti iliyotolewa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa katika Baraza la Usalama la umoja huo imesema kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu ulikiuka vikwazo vya silaha vya umoja huo dhidi ya Libya kwa kuwauzia helikopta na ndege za kivita askari wa Jenerali Khalifa Haftar wanaounga mkono moja kati ya serikali mbili hasimu.

Ripoti hiyo imesema kuwa, Imarati ilitoa misaada ya silaha na kuzidisha uwezo wa anga wa jeshi linaloongozwa na Khalifa Haftar na imekataa kujibu maswali ya wataalamu wa UN.

UN: Imarati imekiuka vikwazo vya Silaha Libya

Jeshi linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar halitambui rasmi serikali ya Umoja wa Kiataifa iliyoko Tripoli ambayo inaungwa mkono na jamii ya kimataifa.

Umoja wa Mataifa ulipiga marufuku aina zote za uuzaji wa silaha kwa Libya baada ya kuondolewa madarakani serikali ya dikteta wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.