Watu 78 wamejeruhiwa katika ghasia za kikabila kusini mwa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30308-watu_78_wamejeruhiwa_katika_ghasia_za_kikabila_kusini_mwa_tunisia
Gavana wa eneo la Qibli kusini mwa Tunisia ametangaza kuwa watu 78 wamejeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea jana katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2017 23:56 UTC
  • Watu 78 wamejeruhiwa katika ghasia za kikabila kusini mwa Tunisia

Gavana wa eneo la Qibli kusini mwa Tunisia ametangaza kuwa watu 78 wamejeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea jana katika eneo hilo.

Gavana wa eneo la Qibli kusini mwa Tunisia ameeleza kuwa mapigano hayo yalisababishwa na hitilafu zilizojitokeza kuhusu umiliki wa ardhi na kwamba pande husika zilitumia silaha katika mapigano hayo ambayo hatimaye yaliingiliwa kati na polisi. Askari usalama mwa Tunisia walifanikiwa kusitisha mapigano hayo kwa kunyunyiza gesi ya kutoa macho na kuwatawanya watu. Maeneo ya vijijini nchini Tunisia yamekuwa yakikumbwa na ghasia za kikabila za kugombea umiliki wa ardhi.