Watu 150 wauawa katika mapigano ya kikabila Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31368-watu_150_wauawa_katika_mapigano_ya_kikabila_nigeria
Mapigano ya kikabila yaliyotokea katika jimbo la Cross River lililoko kusini mashariki mwa Nigeria yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 150.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 05, 2017 09:58 UTC
  • Watu 150 wauawa katika mapigano ya kikabila Nigeria

Mapigano ya kikabila yaliyotokea katika jimbo la Cross River lililoko kusini mashariki mwa Nigeria yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 150.

Gazeti la Premium Times linalochapishwa mjini Abuja limeripoti kuwa, polisi ya jimbo la Cross River imetuma timu ya wataalamu kuchunguza maafa yaliyosababishwa na mapigano hayo ya umwagaji damu. 

Mapigano na hitilafu za makabila na kaumu mbalimbali juu ya malisho ya wanyama nchini Nigeria aghlabu yamekuwa yakisababisha ghasia kubwa kati ya jamii za wafugaji na wakulima. Mapigano kama hayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara katika nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.

Machafuko ya ndani Nigeria

Katika miaka ya hivi karibuni nchi hiyo ya Nigeria imekumbwa na wimbi kubwa la ghasia na machafuko ya kikabila na kikaumu yanayotokana na muundo makhsusi wa jamii ya nchi hiyo.