Al Shabab inawatumia wanawake kama majasusi katika eneo la Pwani Kenya
(last modified Tue, 19 Dec 2017 08:12:09 GMT )
Dec 19, 2017 08:12 UTC
  • Al Shabab inawatumia wanawake kama majasusi katika eneo la Pwani Kenya

Imebainika kuwa wanamgambo wa kundi la al Shabab lenye makao yake nchini Somalia wanatumia mbinu mpya kushambulia kambi za usalama katika maeneo yaliyoainishwa katika oparesheni ya usalama inayoendelea kufanywa na mawakala kadha wa usalama kwa jina la "Linda Boni" huko katika kaunti za Lamu, Tana River na Garissa.

Oparesheni hiyo ilianzishwa mwaka 2015 lengo likiwa ni kuwafurisha magaidi wa al Shabab katika msitu wa Boni na katika maeneo jirani. Wakizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti la Nation, maafisa usalama wanaofanya kazi katika eneo hilo wamesema kuwa magaidi wa al Shabab wanawatumia wanawake kama majasusi katika maeneo yaliyokusudiwa kwenye oparesheni hiyo.

Magaidi wa as-Shabab

Wameongeza kuwa wamekuwa wakichukua hatua za tahadhari hivi sasa mkabala na wanawake hao wanaotumiwa kama majasusi na kwamba  kwa mara kadhaa wamewafukuza wanawake warembo sana ambao waliwahisi kuwa ni majasusi wa kundi la al Shabab. Maofisa hao wameendelea kubainisha kuwa baadhi ya wanawake hao wamekuwa wakijaribu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baadhi ya maafisa.

Tags