Tunisia yapiga marufuku ndege za UAE kutua nchini humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i38047-tunisia_yapiga_marufuku_ndege_za_uae_kutua_nchini_humo
Tunisia imetangaza kupiga marufuku ndege za Shirika la Ndege la Emirates la Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE kutua nchini humo. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya UAE kuwapiga marufuku wanawake wa Tunisia kuingia UAE au kupitia katika ardhi ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Dec 25, 2017 03:17 UTC
  • Tunisia yapiga marufuku ndege za UAE kutua nchini humo

Tunisia imetangaza kupiga marufuku ndege za Shirika la Ndege la Emirates la Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE kutua nchini humo. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya UAE kuwapiga marufuku wanawake wa Tunisia kuingia UAE au kupitia katika ardhi ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Wizara ya Usafiri ya Tunisia imetoa taarifa na kusema: "Imeamuliwa kusimamisha safari zote za Shirika la Ndege la Emirates kutoka na kuingia Tunisia hadi pale shirika hilo litakapozingatia sheria na mikataba ya kimataifa. Shirika la Habari la Tunisia pia limesema Balozi wa UAE mjini Tunis Ijumaa aliitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje kujieleza kufuatia hatua ya wanawake Watunisia kuzuiwa kuingia au kupitia katika ardhi ya UAE..

Mapema Jumapili, waziri msaidizi wa masuala ya kigeni UAE Anwar Gargash alisema uamuzi huo kuhusu wanawake Watunisia ulitokana na sababu za kiusalama.

Shirika la Ndege la Emirates Jumatatu lilitangaza kusitisha safari zake za Tunisia kufuatia agizo hilo la wakuu wa Tunisia.

Uhusiano wa UAE na Tunisia tayari ulikuwa umevurugika kwa sababu kadhaa tokea mwamko wa Kiislamu uanze nchini humo mwaka 2011 na kuenea katika mataifa mengine ya Kiarabu. UAE imekuwa ikiutazama mwamko huo kama tishio kwa ufalme wake na kwa msingi huo imekuwa ikivuruga mchakato wa demokrasia nchini Tunisia ambayo inahesabiwa kuwa ni chimbuko la mwamko wa Kiislamu wa 2011.