Chama kikuu cha upinzani Sudan chamtaka Rais Al Bashir ang'atuke madarakani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i42088-chama_kikuu_cha_upinzani_sudan_chamtaka_rais_al_bashir_ang'atuke_madarakani
Kiongozi wa chama cha Umma nchini Sudan Sadiq al-Mahdi amemtaka rais wa nchi hiyo Omar Hassan Al Bashir aondoke madarakani kwa njia ya amani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 24, 2018 00:08 UTC
  • Chama kikuu cha upinzani Sudan chamtaka Rais Al Bashir ang'atuke madarakani

Kiongozi wa chama cha Umma nchini Sudan Sadiq al-Mahdi amemtaka rais wa nchi hiyo Omar Hassan Al Bashir aondoke madarakani kwa njia ya amani.

Katika tamko la kitisho alilotoa dhidi ya Al Bashir, Sadiq Al Mahdi amemtaka kiongozi huyo ambaye amekuweko madarakani tangu mwaka 1989, aachie hatamu za uongozi wa nchi kwa njia ya amani.

Kiongozi huyo wa chama cha Umma amesema Al Bashir anatakiwa aandae mazingira ya kukabidhi madaraka kwa wananchi, kukomesha mapigano, kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa na kufuta hukumu zote zilizotolewa kisiasa.

Sadiq Al Mahdi

Al Mahdi amesisitiza kuwa wananchi wa Sudan hivi sasa wako tayari zaidi kuanzisha vuguvugu jipya la upinzani wa umma dhidi ya serikali kuliko wakati wowote ule na kuongeza kwamba kuna machaguo kadhaa ya kutumika kwa ajili ya kuipindua serikali, lakini wanafadhilisha kutumia machaguo ya njia za amani.

Kiongozi huyo wa chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini Sudan aidha amesema wito aliotoa rais Al Bashir wa kufanyika uchaguzi ni sawa na kujimaliza kisiasa.

Rais Omar Al Bashir wa Sudan anakabiliwa na mashtaka saba katika Mahakama ya Kimtaifa ya Jinai ICC kuhusiana na mgogoro wa Darfur, matano kati yao yakiwa ni ya jinai dhidi ya binadamu na mengine mawili yanahusiana na jinai za kivita.../