Chama cha Umma chawataka Wasudan kumuondoa madarakani al Bashir
Chama kikuu cha upinzani nchini Sudan kimewataka wananchi na wafuasi wake kumiminika mitaani na kumuondoa madarakani Rais Omar al Bashir wa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho imesema kuwa ni wajibu kwa raia wote wa Sudan kukabilia na serikali ya sasa ya Sudan.
Taarifa hiyo imeashiria hali inayozidi kuwa mbaya ya kichumi, kijamii na kisiasa nchini Sudan na kusisitiza udharura wa kuondolewa madarakani serikali ya sasa ya Khartoum.
Vilevile imezungumzia ukandamizaji wa uhuru wa kiraia na mbinyo wa serikali dhidi ya raia na makundi ya kisiasa, ufisadi na kadhalika ambavyo imesema kuwa vinazidisha hali mbaya ya kiuchumi.
Tangu mwezi Januari mwaka huu Sudan inasumbuliwa na hali mbaya sana ya kiuchumi na uhaba wa fedha wa kigeni na imelazimika hata kufunga baadhi ya balozi zake nje ya nchi.