Watunisia waandamana kupinga njama chafu za Imarati dhidi ya nchi yao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i45822-watunisia_waandamana_kupinga_njama_chafu_za_imarati_dhidi_ya_nchi_yao
Raia wa Tunisia wamefanya maandamano wakipinga njama chafu na uingiliaji wa Imarati katika masuala ya ndani ya nchi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2018 21:54 UTC
  • Watunisia waandamana kupinga njama chafu za Imarati dhidi ya nchi yao

Raia wa Tunisia wamefanya maandamano wakipinga njama chafu na uingiliaji wa Imarati katika masuala ya ndani ya nchi yao.

Maanamano hayo yamefanyika mjini Tunis, mji mkuu wa nchi hiyo ambapo waandamanaji sambamba na kupiga nara dhidi ya Imarati na Lutfi Barham, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo aliyeuzuliwa hivi karibuni kwa kupanga njama ya kutaka kutekeleza mapinduzi ya kijeshi. Ripoti zinasema katika kikao cha siri kilichofanyika hapo tarehe 29 Mei pamoja na mkuu wa idara ya ujasusi wa Imarati katika kisiwa cha Djerba, Tunisia, Barham alishiriki kupanga njama ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Tunis.

oussef Chahed, Waziri Mkuu wa Tunisia

Kakao hicho kilijadili ramani ya njia ya mabadiliko katika uongozi wa juu katika serikali ya Tunisia ikiwemo kumtimua Youssef Chahed, Waziri Mkuu na kumuweka Kamel Marjane mahala pake. Kadhalika katika mazungumzo hayo kulifikiwa mapatano juu ya suala la kumuuzulu Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia. Kufuatia hatua hiyo tarehe sita mwezi huu, Youssef Chahed, Waziri Mkuu wa Tunisia alimpiga kalamu nyekundu Lutfi Barham na kumteua Ghazi al-Jaribi, Waziri wa Vyombo vya Mahakama, kushika nafasi yake.

Barham anatambuliwa kuwa miongoni mwa watu wa karibu kwa dikteta wa zamani wa Tunisia, Zainul Abidin bin Ali aliyekimbilia nchini Saudi Arabia.