Ufaransa yafanya njama za kuhalalisha siasa zake zilizofeli barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i53787-ufaransa_yafanya_njama_za_kuhalalisha_siasa_zake_zilizofeli_barani_afrika
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema kuwa, nchi za eneo la Sahel Africa zisikae muda wote kusubiri msaada wa wanajeshi wa Ufaransa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2019 06:39 UTC
  • Ufaransa yafanya njama za kuhalalisha siasa zake zilizofeli barani Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema kuwa, nchi za eneo la Sahel Africa zisikae muda wote kusubiri msaada wa wanajeshi wa Ufaransa.

Jean-Yves Le Drian ameiambia hayo kamati ya masuala ya nje ya Bunge la Ufaransa na kuongeza kuwa, viongozi wa nchi za eneo la Sahel Africa wasidhani kwamba wanajeshi wa Ufaransa watakuwepo muda wote kwenye eneo hilo.

Ameongeza kuwa usalama wa Afrika inabidi udhaminiwe na Waafrika wenyewe kwani wanajeshi wa Ufaransa hawawezi kuweko milele na milele barani humo.

Matamshi hayo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa yametolewa katika hali ambayo wanajeshi wa nchi hiyo ya Ulaya yenye historia mbaya ya ukoloni barani Afrika walitumwa katika eneo la Sahel Africa mwaka 2013 kwa madai ya kupambana na ugaidi, lakini hadi leo hii wameshindwa kudhamini usalama wa eneo hilo.

Eneo la Sahel Africa

 

Eneo la Sahel Africa limekumbwa na machafuko na mauaji ya mara kwa mara hasa baada ya kupata nguvu magenge ya kigaidi kama vile Daesh na al Qaida katika badhi ya nchi za eneo hilo.

Mwaka 2014 kundi la nchi tano za Sahel Africa za Mali, Niger, Burkina Faso, Chad na Mauritania ziliunda kundi maalumu la ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Tarehe 6 Februari 2017 nchi hizo zilipasisha azimio la kuunda kikosi cha pamoja cha kulinda amani na kupambana na magenge ya kigaidi na misimamo ya kuchupa mipaka.