Jul 19, 2019 02:34 UTC
  • WHO yatangaza Ebola kuwa 'dharura ya kiafya duniani'

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa ni ''dharura ya kiafya inayohitaji jumuia ya kimataifa kuitazama''.

Hatua hiyo inaweza kuzifanya nchi tajiri zinazotoa msaada kutoa fedha zaidi kukabiliana na ugonjwa huo. Lakini shirika hilo limesema hatari ya ugonjwa huo kusambaa nje ya Congo si kubwa.

Uamuzi wa kutangaza ugonjwa wa Ebola kuwa dharura ya kiafya duniani umechukuliwa na jopo la wataalamu wa Shirika la Afya Duniani katika hali ambayo wasiwasi wa kusambaa ugonjwa huo umeongeza zaidi kkatika siku za hivi karibuni.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Shirika la Afya Duniani limezingatia vigezo kadhaa, ambavyo kwanza ni hatari ya kusambaa kwa virusi vya Ebola duniani.

Chanjo ya Ebola

Shirika la Afya Duniani linasema kuuwa, virusi vya ugonjwa huo vinaendelea kusambaa kutoka Afrika magharibi na sasa kufikia nchi nyingine. Mataifa mengi yameimarisha ukaguzi katika viwanja vya ndege.

Wakati huo huo raia wa miji miwili ya Goma mashariki mwa Congo na Gisenyi nchini Rwanda wamezitaka serikali za mataifa hayo mawili kuongeza vifaa vya uchunguzi wa homa ya Ebola kwenye mipaka.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa watu zaidi ya 1,700 wameaga dunia ndani ya miezi 11 iliyopita kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola tangu uripuke upya nchini Kongo DR mwezi Agosti mwaka jana 2018.

Tags