Tunisia yatangaza rasmi tarehe ya uchaguzi wa Rais
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55112-tunisia_yatangaza_rasmi_tarehe_ya_uchaguzi_wa_rais
Viongozi wa Tunisia wametangaza rasmi tarehe 15 mwezi Septemba kuwa siku ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo kufuatia kuaga dunia Rais wa nchi hiyo, Beji Caid Essebsi.
(last modified 2026-02-22T02:21:18+00:00 )
Aug 01, 2019 02:57 UTC
  • Tunisia yatangaza rasmi tarehe ya uchaguzi wa Rais

Viongozi wa Tunisia wametangaza rasmi tarehe 15 mwezi Septemba kuwa siku ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo kufuatia kuaga dunia Rais wa nchi hiyo, Beji Caid Essebsi.

Nabil Bafun Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tunisia amesema kuwa tume hiyo imeainisha tarehe 15 Septemba mwaka huu kuwa siku ya kufanyika uchaguzi wa rais baada ya kushauriana na vyama vya kisiasa. Amesema kuwa wagombea wa kiti cha urais wanapasa kujiandikisha kuanzia tarehe 2 hadi 9 mwezi Agosti na muda wa kufanya kampeni utaanza tarehe 2 hadi 13 Septemba.

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais Tunisia pia yatatangazwa tarehe 17 mwezi huo wa Septemba. Bafun ameongeza kuwa muda wa kufanyika duru ya pili ya uchaguzi huo bado haijaainishwa. Hata hivyo iwapo italazimika kufanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais basi uchaguzi huo utafanyika kabla ya Novemba 3.  

 Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi aliaga dunia katika hospitali ya kijeshi mjini Tunis  tarehe 25 mwezi huu akiwa na umri wa miaka 93 baada ya hali yake ya kiafya kuwa mbaya.  

Mwendazake Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi