Utawala wa Kizayuni unawapatia silaha wanamgambo wa Khalifa Haftar huko Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63201-utawala_wa_kizayuni_unawapatia_silaha_wanamgambo_wa_khalifa_haftar_huko_libya
Maafisa wa jeshi la mashariki mwa Libya wameeleza kuwa mamluki wenye mfungamano na kundi linalojiita " Jeshi la Taifa la Libya" wamepokea maroketi kutoka kwa utawala wa Kizayuni kupitia Imarati.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 03, 2020 11:26 UTC
  • Utawala wa Kizayuni unawapatia silaha wanamgambo wa Khalifa Haftar huko Libya

Maafisa wa jeshi la mashariki mwa Libya wameeleza kuwa mamluki wenye mfungamano na kundi linalojiita " Jeshi la Taifa la Libya" wamepokea maroketi kutoka kwa utawala wa Kizayuni kupitia Imarati.

Duru za kijeshi mashariki mwa Libya; maeneo ambayo yanashikiliwa na Jenerali muasi wa jeshi hilo Khalifa Haftar zimeripoti kuwa shehena mpya ya silaha na zana za kijeshi imewafikia mamluki hao wenye mfungamano na Khalifa Haftar. Maroketi kutoka utawala wa kizayuni aina ya Lynx ni moja ya silaha hizo zilizowafikia wanamgambo wa Jenerali muasi Khalifa Haftar.  

Jenerali muasi, Khalifa Haftar 

Hii si mara ya kwanza kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kuwafikishia  wanamgambo hao wa Jenerali Haftar huko Libya silaha za utawala wa Kizayuni. Huko nyuma pia duru za kijeshi ziliripoti kuwa, Imarati imempatia Jenerali Haftar ndege tatu zisizo na rubani (droni) za utawala ghasibu wa Israel aina ya "Eitan."  

Wanamgambo wanaoongozwa na Khalifa Haftar ambao kwa miaka mingi sasa wanayashikilia maeneo ya mashariki mwa Libya kutokana na uungaji mkono wa hali na mali wanaopata kutoka Saudi Arabia, Misri, Imarati na baadhi ya nchi za Magharibi walianzisha mashambulizi ya kuudhibiti mji mkuu Tripoli tangu Aprili mwaka jana hata hivyo wamegonga mwamba na wameshindwa kufikia lengo lao hilo. Jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kwa upande wao zinaiunga mkono serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al Sarraj.