UN yataka kutekelezwa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63452-un_yataka_kutekelezwa_vikwazo_vya_silaha_dhidi_ya_libya
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kutekeleza vikwazo vya silaha dhidi ya Libya na kuondoka mamluki wote katika nchi hiyo ya Kiafrika.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 16, 2020 07:47 UTC
  • UN yataka kutekelezwa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kutekeleza vikwazo vya silaha dhidi ya Libya na kuondoka mamluki wote katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana usiku lilipasisha azimio hilo kwa kura 13 za ndio. China na Russia hazikulipigia kura azimio hilo. Baraza la Usalama aidha limesisitiza udharura wa kufanyika mazungumzo ya kisiasa nchini Libya na kusitishwa mapigano ya ndani. 

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamezituhumu pande zinazozozana nchini Libya na nchi ajinabi zinazounga mkono vita nchini humo kwa kukiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na kueleza kuwa: Kufuatia misaada ya moja kwa moja ya Uturuki na Imarati, utumaji wa silaha wa nchi hizo huko Libya umeongeza; hatua ambayo inakiuka vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa.  

Libya ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani baada ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wale wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia nchi hiyo na kusaidia harakati za kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011. 

Kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi 

Libya sasa imegawanyika katika maeneo mawili.