Antonio Guterres: Mustakbali wa Libya upo hatarini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63858-antonio_guterres_mustakbali_wa_libya_upo_hatarini
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyahimiza mataifa makubwa duniani yenye maslahi katika vita vinavyoendelea huko Libya kuacha kuzitumia silaha serikali waitifaki wao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 06, 2020 12:12 UTC
  • Antonio Guterres: Mustakbali wa Libya upo hatarini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyahimiza mataifa makubwa duniani yenye maslahi katika vita vinavyoendelea huko Libya kuacha kuzitumia silaha serikali waitifaki wao.

Antonio Guterres amesema kuwa mustakbali wa Libya upo hatarini na kwamba mataifa yote makubwa ulimwengu ambayo yana maslahi katika vita vya ndani vya muda mrefu huko Libya yanapasa kuacha kuzitumai silaha serikali waitifaki wao hukoLibya na badala yake yafanye juhudi za kufanikisha amani ya kudumu nchini humo.

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, ukiukaji wa vikwazo vya silaha ilivyowekewa Libya ni uhalifu na akahoji kuhusu azma kuu ya pande zote husika kuhusu amani ya Libya.

Ujerumani ambayo imekuwa ikijaribu kuwa msuluhishi katika mgogoro wa Libya imesema kuwa mkutano wa ngazi ya mawaziri uliofanyika jana kwa kuitishwa na Umoja wa Mataifa na Ujerumani kusaidia juhudi za kusaka amani huko Libya ilikuwa ni fursa ya kupitia yale yote yaliyofikiwa tangu kufanyika Mkutano wa Berlin kuhusu Libya mwezi Januari mwaka huu. Katika mkutano huo, washiriki kutoka pande zote husika katika mgogoro wa Libya zilikubaliana kuheshimu vikwazo vya silaha na kuzishawishi pande zinazozozana nchini humo kufikia usitishaji vita kamili. Hata hivyo makubaliano hayo ya Berlin yamekiukwa.