UN yalaani kushambuliwa madaktari wasio na mipaka CAR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9661-un_yalaani_kushambuliwa_madaktari_wasio_na_mipaka_car
Umoja wa Mataifa umelaani kushambuliwa msafara wa madaktari wasio na mipaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 21, 2016 03:13 UTC
  • UN yalaani kushambuliwa madaktari wasio na mipaka CAR

Umoja wa Mataifa umelaani kushambuliwa msafara wa madaktari wasio na mipaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Dr. Michel Yao amelaani vikali mashambulizi hayo dhidi ya msafara wa madaktari hao wenye kutoa misaada ya kibinadmau. Shambulio la kwanza lilifanyika Juni 17 kati ya eneo la Sibut na Grimari mjini Kemo ambapo mkuu wa msafara aliuawa huku wafanyakazi wengine wakifanikiwa kukimbilia msituni. Waliotekeleza shambulio hilo ni watu wenye silaha wasiojulikana. Msafara huo ulikuwa unasafirisha dawa na mafuta kutoka mji mkuu Bangui kuelekea Bangassou.

Dr. Yao amesema shambulio lingine lilitokea karibu na Bossangoa Juni 18 ambapo aliuawa dereva wa shirika hilo la madaktari wasio na mipaka.

Ameongeza kuwa mashambulio hayo ya kikatili yanadhihirisha hali halisi ya kutokuwepo kwa usalama barabarani jambo ambalo linafanya kuwa ngumu sana kazi ya watoa misaada ya kibinadamu kwa maelfu ya watu wanaohitaji msaada huo.