Raisi: Marekani na Israel zinakula njama za kuvuruga usalama wa eneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i100874-raisi_marekani_na_israel_zinakula_njama_za_kuvuruga_usalama_wa_eneo
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikosi vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Kiislamu si tu vinalinda usalama wa taifa hili, bali pia usalama na uthabiti wa nchi nyingine za eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 09, 2023 08:43 UTC
  • Raisi: Marekani na Israel zinakula njama za kuvuruga usalama wa eneo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikosi vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Kiislamu si tu vinalinda usalama wa taifa hili, bali pia usalama na uthabiti wa nchi nyingine za eneo la Asia Magharibi.

Rais Ebrahim Raisi amesema hayo leo katika marasimu ya kuwakumbuka na kuwaenzi Walinzi wa Harama Tukufu ambao waliuawa shahidi na kumwaga damu zao kwa ajili ya kudhamini usalama wa Iran na nchi za eneo.

Sayyid Raisi ameeleza bayana kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinataka kuvuruga usalama wa eneo hili kupitia njama zao, lakini hata hivyo kuwa njama hizo zimefeli na kugonga mwamba.

Rais wa Iran amekumbusha kuwa, ujumbe wa Mashahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ni kutaka kudumishwa muqawama na mapambano dhidi ya maadui na njama zao. 

Amesema utamaduni wa kujitoa muhanga na kufa shahidi katika mapambano dhidi ya dhulma unaandaa mazingira ya kurejea muokozi aliyeahidiwa, Imam Mahdi (AF) na kuimarika ustaarabu mpya wa Kiislamu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, vikosi vya ulinzi na usalama vya Iran vitaendelea kujitolea kwa dhati kudhamini usalama wa taifa hili na pia wa nchi nyingine za eneo la Asia Magharibi, mkabala wa njama za maadui.

Sayyid Raisi ameongeza kuwa, "Kila tulicho nacho leo hii kimetokana na kujitolea muhanga Mashahidi. Iran inadumisha usalama popote inapoenda."