Iran: Mapinduzi, vikwazo ni vyombo vya mabeberu vya kuyakandamizi mataifa huru
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101264-iran_mapinduzi_vikwazo_ni_vyombo_vya_mabeberu_vya_kuyakandamizi_mataifa_huru
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, madola ya kibeberu na ya kiistikbari yanatumia kila njia kuyakandamiza mataifa huru duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 19, 2023 23:26 UTC
  • Iran: Mapinduzi, vikwazo ni vyombo vya mabeberu vya kuyakandamizi mataifa huru

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, madola ya kibeberu na ya kiistikbari yanatumia kila njia kuyakandamiza mataifa huru duniani.

Hossein Amir-Abdollahian amesema, "Ushawishi, mapinduzi ya kijeshi, vikwazo vya kiuchumi, mapigano na vita laini ni miongoni mwa vyombo vinavyotumiwa na madola ya kibeberu kukandamiza azma ya nchi huru duniani." 

Abdollahian amesema hayo katika ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter) jana Jumamosi, kwa mnasaba wa kutimia miaka 70, tangu yatokee mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 19, 1953 (Mordad 28, 1332), ambayo yalipelekea kupinduliwa serikali ya Waziri Mkuu wa Iran wakati huo Mohammad Mosaddegh.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ameeleza bayana kuwa, mapitio ya historia ya mapinduzi yanaonesha kuwa, ukoloni wa zamani na ukoloni mamboleo una hulka moja ambayo daima ipo dhidi ya mataifa huru duniani.

Serikali ya Uingereza ilikuwa ndiye mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo ya Mordad 28, na Marekani ilitoa mchango muhimu na athirifu katika kufanikisha mpango huo. Kuuzuliwa kwa Mosaddegh kulikofanyika miaka 70 iliyopita yalikuwa matokeo ya njama na hatua za pamoja zilizochukuliwa na mashirika ya kijasusi ya CIA ya US na MI6 ya UK.

Hapo jana pia, Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema kupanga na kufadhili mapinduzi, kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na kuwaunga mkono madikteta ni katika sera kuu za Marekani na Uingereza katika kipindi chote cha historia.