Mar 17, 2024 11:10 UTC
  • Mashirika 16 ya Kiirani katika maonyesho ya afya Kenya

Mashirika 16 ya ubunifu wa utaalamu ya Iran yanashiriki katika duru ya 24 la Maonyesho ya Sekta ya Afya nchini Kenya, yaliyopangwa kufanyika Nairobi kuanzia tarehe 17 hadi 19 mwezi Aprili mwaka huu.

Maonyesho ya 24 ya Afya ya Kenya ambayo yatahudhuriwa na nchi zaidi ya 35 duniani kwa lengo la kuondoa ombwe na mapengo yaliyopo ni fursa nzuri ya kuonyesha ubunifu wa hivi karibuni na kuimarisha uhusiano wa kibiashara nje ya nchi, hasa katika bara la Afrika. 

Shirika la habari la Mehr limemnukuu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na sayansi, teknolojia na uchumi wa ubunifu wa utaalamu akisema kuwa mashirika 16 ya ubunifu wa utaalamu ya Iran yataonyesha bidhaa na uwezo wao katika nyanja tatu za madawa, vifaa tiba na suhula za maabara katika Maonyesho ya 24 ya Afya huko Kenya. 

Maonyesho ya sekta ya afya Kenya,2023 

Ripoti zinasema, miongoni mwa huduma zitakazotolewa kwa mashirika yatakayoshiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na mipango muhimu ya kufanya mazungumzo ya biashara na wateja wakubwa, kutembelea mahospitali na sekta ya binafsi inayofanya kazi katika uwanja huu.

Katika miaka ya karibuni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeingia katika masoko ya kimataifa ikiwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kufanikiwa kusafirisha bidhaa mbalimbali katika nchi nyingine za dunia.

Tags