May 28, 2024 08:18 UTC
  • Wabunge wamchagua Qalibaf kuwa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge)

Wawakilishi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) wamemchagua Muhammad Bagheri Qalibaf kuwa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu katika mkutano wa kwanza wa bunge la 12.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, kikao cha leo cha duru ya 12 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran, kimemchagua Muhammad Qalibaf mwakilishi wa Tehran kuwa Spika. Muhammad Bagheri Qalibaf amefanikiwa kuwashinda wagombea wenzake ambao ni Hujattul Islam wal Muslimin Mujtaba ZulNur mgombea kutoka mji wa Qum na Manochehjr Mutaki kutoka Tehran. 

Baada ya kupiga kura kwa njia ya karatasi, Muhammad Bagheri Qalibaf aliiibuka na ushindi kwa kupata kura 198 kati ya jumla ya kura 287 za wakilishi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran.  

Hafla ya ufunguzi wa duru ya 12 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ilifanyika jana kwa kuhudhuriwa na wabunge waliochaguliwa pamoja na viongozi wa serikali na jeshi.  

Bunge la 12 la Iran lilizinduliwa hana kwa ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei. 

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi  

Kiongozi Muadhamu alisisitiza umuhimu wa kuendelea na kuimarisha "demokrasia ya kidini", akisema kuwa ni "zawadi kubwa ya Mwenyezi Mungu" kwa taifa la Iran.

Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa kila mwakilishi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ni mwakilishi wa nchi nzima suala linalomaanisha kuwa kazi kuu ya wabunge ni kulinda maslahi ya taifa.

 

Tags