Kiongozi Muadhamu: Muqawama ni utambulisho mzuri sana wa Syria
(last modified Thu, 30 May 2024 13:02:07 GMT )
May 30, 2024 13:02 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Muqawama ni utambulisho mzuri sana wa Syria

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muqawama ni utambulisho mzuri na bora wa Syria na akaeleza kwamba, nafasi maalumu iliyonayo Syria katika eneo ni kutokana na utambulisho huu na sifa hiyo muhimu inapaswa kuhifadhiwa.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Rais Bashar Assad wa Syria na ujumbe alioandamana nao. Kiongozi Muadhaamu amelitathmini suala la kuimarishwa uhusiano kati ya Iran na Syria kuwa muhimu, kwa kuzingatia kuwa nchi hizo mbili ndio mhimili wa muqawama na kusema: Utambulisho wa mzuri wa Syria. , ambao ndio ule muqawama na mapambano uliokuweko tangu zama za marehemu Hafez Assad  na kuwekwa jiwe la msingi la "Kambi ya Muqawama na Kusimama Kidete"  utambulisho ambao daima umesaidia umoja wa kitaifa wa Syria.

Akisisitiza haja ya kuhifadhiwa utambulisho huo, Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: Wamagharibi na wafuasi wao katika eneo walianzisha vita dhidi ya Syria kwa minajili ya kuupindua mfumo wa kisiasa wa Syria na kuiondoa nchi hiyo katika mahesabu ya kieneo lakini hawakufanikiwa na sasa wanapanga mbinu nyingine, ikiwa ni pamoja na ahadi ambazo hazitatimizwa kamwe, ili kuiondoa Syria katika mahesabu ya kikanda.

Mazungumzo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na Rais wa Syria Bashar al-Assad

 

Ayatullah Khamenei ameashiria mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi ya Marekani na Ulaya dhidi ya Iran na Syria na akasema: Ni lazima tuyashinde mazingira haya kwa kuzidisha ushirikiano na kuyaweka ushirikiano huu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amekosoa misimamo dhaifu ya baadhi ya nchi za eneo kuhusiana na kadhia ya Gaza na akaashiria kikao cha hivi karibuni cha viongozi wa nchi za Kiarabu kilichofanyika mjini Manama na kuongeza kuwa: Katika kikao hicho kulifanyika uzembe mwingi kuhusu Palestina na Gaza, lakini baadhi ya nchi pia zilifanya vyema.

Tags