Waziri wa Ulinzi wa Iran: Mfumo wa ulinzi wa Marekani wa THAAD si jambo jipya
(last modified Thu, 17 Oct 2024 02:55:08 GMT )
Oct 17, 2024 02:55 UTC
  • Waziri wa Ulinzi wa Iran: Mfumo wa ulinzi wa Marekani wa THAAD si jambo jipya

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza kuwa mfumo wa ulinzi wa Marekani wa THAAD si jambo jipya na kwamba Iran unalichukulia suala hilo kuwa ni sehemu ya vita vya kisaikolojia na sio tatizo mahsusi.

Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh alisema jana Jumatano pambizoni mwa kikao cha serikali akijibu swali kuhusu iwapo makombora ya Iran yanaweza kuuvuka mfumo wa ulinzi wa Marekani wa THAAD ambao Washington inatazamia kuupa Tel Aviv kwamba: 'Mfumo wa THAAD ambao ni moja ya mifumo ya kutungua makombora ya balistiki si jambo jipya na kuwa ulikuwepo pia huko nyuma.'

Mfumo wa THAAD 

Aziz Nasirzadeh ameeleza kuwa tunaitathmini kadhia hii kuwa ni vita vya kisaikolojia na si tatizo mahsusi. Ameongeza kuwa vitisho vya utawala ghasibu wa Israel si suala geni na kuwa vitisho hivyo vimekuwa vikitolewa mara kwa mara.

Mfumo wa ulinzi wa makombora wa Marekani wa (THAAD) ni ufupisho wa Terminal High-Altitude Area Defence. Mfumo huo wa ulinzi wa makombora unaweza kuyafuatilia na kuyanasa makombora ya masafa mafupi na ya kati katika anga hewa ya ndani na nje katika hatua ya mwisho ya kuruka au pale yanapoelekea kupiga shabaha iliyokusudiwa. 

Hivi karibuni, Marekani imekubali ombi la utawala wa Kizayuni la kuupatia mfumo huo wa ulinzi wa makombora.

Tags