Iran yapinga vikali taarifa ya GCC
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i2374-iran_yapinga_vikali_taarifa_ya_gcc
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali taarifa iliyotolewa na Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi inaliyoitambua harakatri ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 03, 2016 14:30 UTC
  • Iran yapinga vikali taarifa ya GCC

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali taarifa iliyotolewa na Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi inaliyoitambua harakatri ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi.

Hussein Jabiri Ansari amesema kuwa, harakati hiyo imekuwa nembo ya mapambano dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel kutokana na kusimama kwake kidete mbele ya wavamizi wa kuwaunga mkono kwa pande zote wanancdhi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Jabiri Ansari amesema kuwa upinzani wa baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya harakati ya Hizbullah ambayo ni mwakilishi wa thamani na matukufu ya Umma wa Kiislamu katika kupigania uhuru, kujitawala na uadilifu na kupambana na makundi ya kigaidi na yenye misimamo ya kufurutu mipaka unaonesha jinsi nchi hizo zinavyoshirikiana na Wazayuni maghasibu wanaoikalia kwa mabavu Palestina.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa viongozi wanaoeneza uongo na propaganda na kuweka mashinikizo dhidi ya nchi nyingine kwa ajili ya kueneza misimamo yao wanafanyakazi dhidi ya maslahi ya nchi za Kiislamu kwa kujua au bila ya kujua.

Baraza la Ushirikiano wa Ghuba wa Ujamemi jana Jumatano liliiweka harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika orodha ya makundi ya kigaidi na kutangaza kuwa, imechukua hatua kadhaa katika uwanja huo. Hatua ya baraza hilo linaloundwa na nchi za Saudi Arabia, Qatar, Kuwait, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain umekabiliwa na upinzani mkubwa ndani ya nje ya Lebanon.