Mdahalo wa tatu wa wagombea urais Iran kufanyika Ijumaa Alasiri
(last modified Fri, 12 May 2017 05:44:33 GMT )
May 12, 2017 05:44 UTC
  • Mdahalo wa tatu wa wagombea urais Iran kufanyika Ijumaa Alasiri

Mdahalo wa tatu na wa mwisho wa wagombea sita wa kiti cha urais wa awamu ya 12 katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utafanyika leo saa kumi na nusu kwa majira ya Tehran .

Mdahalo huo utarushwa hewani kwa njia ya moja kwa moja kupitia Kanali ya Kwanza ya Televisheni ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu la Iran IRIB. Aidha mdahalo huo unatazmiwa akurushwa hewani kote duniani kupitia kanali ya televisheni ya Kiingereza ya Press TV na pia Al Alam kwa lugha ya Kiarabu. Mdahalo wa leo utajikita katika masuala ya uchumi baada ya midahalo miwili iliyopita ambayo ilijumuisha masuala ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Wagombea urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwaka 2017

Wagombea sita wa urais mwaka huu ni pamoja na Mostafa Aqa-Mirsalim ambaye ni waziri wa zamani wa utamaduni na muongozo wa Kiislamu, Mostafa Hashemi-Taba makamu wa rais wa zamani ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa kamati ya taifa ya Olimpiki, Es'haq Jahangiri makamu wa kwanza wa serikali ya sasa, Mohammad-Baqer Qalibaf meya wa mji wa Tehran, Seyyed Ebrahim Raeisi msimamizi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS na rais wa hivi sasa, Hassan Rouhani ambaye anatetea nafasi yake ili amalize kipindi chake cha pili.

Uchaguzi wa 12 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya tarehe 19 mwezi ujao wa Mei sambamba na uchaguzi wa tano wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji kote nchini Iran. 

Kamati ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema Wairani zaidi ya milioni 56 wametimiza masharti yote ya kupiga kura na hivyo wanatazamiwa kushiriki katika uchaguzi ujao wa urais.

Wairani wanaoishi nje ya nchi wataweza kupiga kura katika vituo 269 vya upigaji kura vilivyoko katika ofisi 131 za kidiplomasia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi 103 kote duniani.

Uchunguzi wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB hivi karibuni ulioyesha kuwa, takriban asilimia 70.6 ya wananchi wa Iran waliotimiza masharti ya kupiga kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wa 12 wa rais humu nchini.

Tags