Zarif: Upayukaji wa Trump hauwezi kutia doa istikama ya wananchi wa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i35910-zarif_upayukaji_wa_trump_hauwezi_kutia_doa_istikama_ya_wananchi_wa_iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema jana usiku mbele ya Wairani wanaoishi Afrika Kusini kwamba, upayukaji wa rais wa Marekani Donald Trump hauwezi kutia doa hata chembe katika ulinzi, muqawama na heshima ya wananchi wa Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 24, 2017 04:05 UTC
  • Zarif: Upayukaji wa Trump hauwezi kutia doa istikama ya wananchi wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema jana usiku mbele ya Wairani wanaoishi Afrika Kusini kwamba, upayukaji wa rais wa Marekani Donald Trump hauwezi kutia doa hata chembe katika ulinzi, muqawama na heshima ya wananchi wa Iran.

Tarehe 13 Oktoba, Donald Trump alirejea kutoa matamshi yake ya kipunguwani dhidi ya taifa la Iran kwa kudai kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran eti inaunga mkono ugaidi wakati anatambua vyema kwamba Iran imekuwa na mchango mkubwa katika vita dhidi ya magaidi wanaoungwa mkono na Marekani katika nchi za Syria na Iraq.

Iran imeitikia ombi rasmi la serikali za Iraq na Syria zilizoomba msaada wa Tehran katika kupambana na magaidi na ndio maana ikatuma washauri wake wa kijeshi katika nchi hizo kuwasaidia wananchi wa Iraq na Syria kujipapatua kutoka katika makucha ya magaidi makatili wanaoungwa mkono kwa kila hali na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mohammad Javad Zarif katika mazungumzo na Wairani waishio Afrika Kusini

 

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Dk Mohammad Javad Zarif akisema kuwa, kwa uungaji mkono wa wananchi, Iran ya Kiislamu imeweza katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, kukabiliana na mashinikizo yote, uvamizi na vikwazo vyote vya mabeberu dhidi yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Tehran haina deni la nchi yoyote katika maendeleo yake ya kiuchumi na kielimu na kwamba hakuna nchi yeyote yenye utulivu na usalama kama Iran katika eneo hili.

Amezungumzia pia jinai zinazofanywa na Saudi Arabia na kundi lake dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Yemen na kusema, utawala wa Saudia unatumia dola za mafuta kununua marundo ya silaha za Marekani na baadaye kuzitumia kuwashambulia kinyama wananchi wanaodhulumiwa wa Yemen.