Rais wa Austria: Iran ni nchi kubwa katika Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i4033-rais_wa_austria_iran_ni_nchi_kubwa_katika_mashariki_ya_kati
Rais Heinz Fischer wa Austria amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nchi kubwa katika eneo lenye mivutano la Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 29, 2016 14:18 UTC
  • Rais wa Austria: Iran ni nchi kubwa katika Mashariki ya Kati

Rais Heinz Fischer wa Austria amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nchi kubwa katika eneo lenye mivutano la Mashariki ya Kati.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kwa mnasaba wa kukaribia safari ya Rais Hassan Rouhani nchini Austria itakayofanyika hapo kesho, Heinz Fischer amesema historia ya uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Austria inarejea kipindi cha miaka mingi nyuma.

Rais wa Austria amebainisha kuwa Iran ni nchi kubwa katika eneo lenye mivutano la Mashariki ya Kati; na dunia inaweza kupunguza mivutano hiyo hadi kiwango cha chini kwa kushirkiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha ameashiria safari yake iliyofana hapa nchini na mazungumzo aliyofanya na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais, Spika wa Bunge na viongozi wengine, na kusisitiza kuwa safari ya Rais Rouhani huko Austria inaweza kusaidia sana kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili.

Rais Heinz Fischer wa Austria ameongeza kuwa nchi yake ina hamu ya kustawisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja zote ikiwemo kushirikiana katika sekta za nishati, uchumi, sayansi na elimu.../