Ayatullah Khamenei: Sera za uchumi ngangari zitekelezwe ipasavyo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i4576-ayatullah_khamenei_sera_za_uchumi_ngangari_zitekelezwe_ipasavyo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amekutana na kuhutubia hadhara ya maafisa wa mihimili mitatu ya dola na kusisitiza kuwa ataunga mkono kwa nguvu zote hatua yoyote yenye manufaa na ya dharura kwa ajili ya maslahi ya taifa, na kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 07, 2016 02:50 UTC
  • Ayatullah Khamenei: Sera za uchumi ngangari zitekelezwe ipasavyo

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amekutana na kuhutubia hadhara ya maafisa wa mihimili mitatu ya dola na kusisitiza kuwa ataunga mkono kwa nguvu zote hatua yoyote yenye manufaa na ya dharura kwa ajili ya maslahi ya taifa, na kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.

Hotuba ya Kiongozi Muadhamu imejikita zaidi kwenye utekelezaji wa sera za uchumi ngangari kwa ajili ya kutatua matatizo ya kiuchumi baada ya makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1. Ayatullah Khamenei ametoa wito wa kuanzishwa kambi ya uchumi ngangari na kusema kuwa: Kambi hiyo inapaswa kuongozwa na serikali na haswa Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye kwa ushirikiano wa asasi zote na kulipa umuhumi zaidi suala la uzalishaji wa ndani, inaweza kutayarisha uwanja mzuri wa harakati ya pande zote kwa ajili ya kuchukuliwa hatua na matendo katika suala la uchumi ngangari. Ayatullah Khamenei amesema kuwa, kuna ulazima wa kuimarisha zaidi asasi zinazopiga hatua katika njia ya siasa na sera hiyo na kuzielekeza katika njia sahihi zile zisizokuwa katika njia hiyo.

Tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya aina mbalimbali ya kiuchumi. Sehemu kubwa ya matatizo hayo inatokana na siasa za Marekani na nchi za Magharibi kwa ajili ya kutoa dharba kwa uchumi wa Iran. Maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu walidhani kwamba, wangeweza kudhoofisha mapinduzi hayo kwa kuanzisha matatizo ya kiuchumi na kuibana Iran katika kuingia katika masoko ya kimataifa. Katika kipindi chote cha miongo mitatu iliyopita nchi za Magharibi zimeiwekea Iran aina mbalimbali ya vikwazo. Marekani na waitifaki wake hususan katika muongo mmoja wa hivi karibuni waliiwekea Jamhuri ya Kiislamu vikwazo vikali zaidi na visivyo na kifani katika historia ya Umoja wa Mataifa kwa kupasisha maazimio kadhaa dhidi ya Iran kwa kisingizio kuwa miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia hapa nchini ina malengo ya kijeshi.

Kinyume na matarajio ya maadui, siasa hizo hazikuwafanya wananchi wa Iran kujitenga na Mfumo wa utawala wa Kiislamu, bali hata katika chaguzi kadhaa zilizopita hususan uchaguzi wa Rais uliofanyika miaka mitatu iliyopita, wananchi walishiriki kwa asilimia 70 katika zoezi hilo na kuonesha uungaji mkono wao kwa demokrasia ya kidini ya Iran. Katika uchaguzi huo Dakta Hassan Rouhani, aliyehudumu katika ngazi mbalimbali za serikali kwa kipindi cha miongo mitatu na kuwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa kwa kipindi cha miaka 16, alishinda uchaguzi na kuchaguliwa na wananchi kuwa Rais wa Jamhuri. Dakta Rouhani alitangaza waziwazi kwamba moja kati ya ajenda kuu za serikali yake ni kuondoa vikwazo vya kidhamu vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Iran kwa kisingizio cha miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia hapa nchini. Timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran baada ya mazungumzo magumu ya miaka miwili na kundi la 5+1 iliweza kutia saini mapatano yaliyohitimisha vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi na wakati huo huo kudumisha shughuli za kuzalisha nishati ya nyuklia hapa nchini.

Serikali ya Marekani pia inaweka vikwazo katika utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia yaliyopasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo inapasa kueleweka kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikuegemeza uchumi wake kwenye uhusiano na madola ya Magharibi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kwa kutilia maanani tabia ya nchi za Magharibi ya kukiuka mikataba na makubaliano mbalimbali, Iran inapaswa kuchukua sera zitakazolinda uchumi wake mbele ya vitisho na vikwazo vya maadui.

Ni kwa msingi huo ndipo Ayatullah Ali Khamenei akasisitiza kuwa uchumi ngangari na unaotegemea uwezo wa ndani kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya kiuchumi ndiyo njia pekee ya kuwa imara mbele ya vitisho na vikwazo vya maadui wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.