Iran: Hatua ya Bunge la Canada dhidi yetu ni kosa la kistratijia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i45804-iran_hatua_ya_bunge_la_canada_dhidi_yetu_ni_kosa_la_kistratijia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Bahram Qassemi ametoa radiamali kufuatia muswada wa kutaka kuweka vizingiti kwenye mahusiano ya nchi hii katika Bunge la Canada na kusema kuwa muswada huo ni kosa kubwa la kistratijia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 13, 2018 15:41 UTC
  • Iran: Hatua ya Bunge la Canada dhidi yetu ni kosa la kistratijia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Bahram Qassemi ametoa radiamali kufuatia muswada wa kutaka kuweka vizingiti kwenye mahusiano ya nchi hii katika Bunge la Canada na kusema kuwa muswada huo ni kosa kubwa la kistratijia.

Bunge la Canada Jumanne ya jana sambamba na kuwasilisha muswada huo, liliitaka serikali ya nchi hiyo kusimamisha aina yoyote wa mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa kisiasa baina ya nchi mbili. 

Bahram Qassemi amelaani muswada huo wa Bunge la Canada na kusema kuwa, kuwasilishwa kwake bungeni kumetokana na kukosa uelewa kamili na wa kutosha wa baadhi ya wabunge wa nchi hiyo kuhusiana na misimamo ya wazi na ya mantiki ya Iran ya Kiislamu katika kukabiliana na ugaidi.

Bunge la Canada

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebainisha kwamba, fikra za walimwengu haziwezi kukubaliana na tuhuma za kubuni na zisizo na ukweli wowote kwamba eti Tehran inaunga mkono ugaidi. Ameongeza kwamba, katika miongo kadhaa iliyopita raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walikuwa wahanga wakubwa wa vitendo vya ugaidi ambao ulikuwa unaongwa mkono na nchi zinazojulikana katika uwanja huo. 

Qassemi amesisitiza kwamba raia wa Iran na kwa kutegemea misingi ya tabia njema na mafundisho ya kidini na kiutamaduni, daima wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na makundi ya kufurutu ada na ya kiugaidi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameonya juu ya matokeo mabaya ya kupasishwa muswada huo.