Brigedia Jenerali Hatami: Israel ni tishio kwa usalama wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46452-brigedia_jenerali_hatami_israel_ni_tishio_kwa_usalama_wa_kimataifa
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia shambulio la silaha za kemikali lililofanywa miaka kadhaa iliyopita na utawala wa Saddam Hussein dhidi ya mji wa Sardashti kaskazini magharibi mwa Iran na kusisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kwa usalama wa kimataifa kutokana na kumiliki kwake silaha zilizopigwa marufuku.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 30, 2018 04:09 UTC
  • Brigedia Jenerali Hatami: Israel ni tishio kwa usalama wa kimataifa

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia shambulio la silaha za kemikali lililofanywa miaka kadhaa iliyopita na utawala wa Saddam Hussein dhidi ya mji wa Sardashti kaskazini magharibi mwa Iran na kusisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kwa usalama wa kimataifa kutokana na kumiliki kwake silaha zilizopigwa marufuku.

Tarehe 28 mwezi Juni mwaka 1987 iliyosadifiana na tarehe 7 mwezi Tiir mwaka 1366 Hijria Shamsia, utawala wa Baath wa Iraq uliushambulia mji wa mpakani wa Iran wa Sardashti na kuwauwa shahidi raia wa mji huo 119 na kuwajeruhi wengine zaidi ya elfu nane ambao walidhurika na silaha hizo za kemikali.  

Wahanga wa shambulio la kemikali katika mji wa Sardashti, Iran mwaka 1987 

Brigedia Jenerali Amir Hatami leo Ijumaa ametuma ujumbe akiashiria hatua ya kuzuia ukaguzi na kuharibiwa silaha za kemikali za utawala ghasibu wa Israel ambao ndio tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama wa eneo hili na kutahadharisha kuhusu ugaidi wa kikemikali katika eneo la Asia magharibi.  

Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mhanga mkuu wa silaha za kemikali na kuongeza kuwa bado kuna wasiwasi kuhusu amani na usalama wa eneo hili baada ya kupita miongo miwili tangu kuasisiwa shirika linalopiga marufuku silaha za kemikali (OPCW).  

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameendelea kubainisha kuwa: Marekani ilikiuka sheria za kimataifa na kulipuuza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na shirika la OPCW kwa kuishambulia miundo mbinu ya serikali ya Syria kwa kisingizio cha kutumiwa silaha za kemikali na hivyo ikazidisha machafuko na ukosefu wa amani katika eneo la Asia magharibi.