Bahram Qassemi: Saudia ni chanzo na muungaji mkono mkuu wa ugaidi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i48476-bahram_qassemi_saudia_ni_chanzo_na_muungaji_mkono_mkuu_wa_ugaidi_duniani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa chanzo cha ugaidi ambao hii leo umeitumbukiza dunia katika matatizo hususan eneo la Mashariki ya Kati, si mahala pengine ghairi ya Saudi Arabia kupitia fikra na misimamo ya kufurutu ada inayoenezwa na kudhaminiwa kifedha na utawala wa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Sep 29, 2018 21:57 UTC
  • Bahram Qassemi: Saudia ni chanzo na muungaji mkono mkuu wa ugaidi duniani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa chanzo cha ugaidi ambao hii leo umeitumbukiza dunia katika matatizo hususan eneo la Mashariki ya Kati, si mahala pengine ghairi ya Saudi Arabia kupitia fikra na misimamo ya kufurutu ada inayoenezwa na kudhaminiwa kifedha na utawala wa nchi hiyo.

Bahram Qassemi, ameyasema hayo wakati akijibu madai yasiyo na msingi na  ya kila siku ya Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia aliyoyatoa katika mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kuongeza kuwa, suala la al-Jubeir kujifakharisha kwamba nchi yake ni muungaji mkono mkubwa wa stratijia za rais wa Marekani, Donald Trump katika kupambana na nchi nyingine au kuharibu makubaliano ya kimataifa, si jambo la ajabu kwani Saudi Arabia kwa kushirikiana na lobi za Kizayuni na utawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), zinatumia mabilioni ya dola kwa ajili ya kuzielekeza siasa za Marekani kwenye vita na kuzusha ghasia kwa maslahi yao. 

Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria namna Saudia ilivyounda muungano vamizi wa kijeshi dhidi ya nchi ya Waislamu ya Yemen na kusema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi vamizi, inayohusika na uharibifu na mauaji ya umati dhidi ya wananchi madhlumu wa Yemen, akitumia vibaya jukwaa la Umoja wa Mataifa katika kueneza misimamo mikali, chuki, ukatili na kupiga ngoma ya vita, anasukumwa na fikra na mafundisho hatari aliyoyapata chini ya malezi ya utawala wa Aal-Saud. Siku ya Ijumaa Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia alidai katika mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba, eti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inahusika na machafuko katika eneo la Mashariki ya Kati na kwamba Saudia inaunga mkono stratijia mpya ya Marekani kwa ajili ya kukabiliana na Tehran.