Larijani: Uingereza imelazimika kulegeza msimamo mkabala na nguvu ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55428-larijani_uingereza_imelazimika_kulegeza_msimamo_mkabala_na_nguvu_ya_iran
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia suala la kuachiwa meli ya mafuta ya Iran ya Grace-1 na kueleza kuwa Uingereza imelazimika kusalimu amri mbele ya nguvu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 17, 2019 02:28 UTC
  • Larijani: Uingereza imelazimika kulegeza msimamo mkabala na nguvu ya Iran

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia suala la kuachiwa meli ya mafuta ya Iran ya Grace-1 na kueleza kuwa Uingereza imelazimika kusalimu amri mbele ya nguvu ya Iran.

Tarehe nne mwezi Julai mwaka huu wanajeshi wa kikosi cha majini cha Uingereza waliisimamisha  na kuikamata meli ya mafuta ya Iran ya Grace-1 katika Lango bahari la Gibraltar kwa kisingizio kisicho na msingi cha kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhdi ya Syria. Mahakama Kuu ya eneo la Gilbraltar juzi Alhamisi iliagiza kuachiwa huru meli hiyo ya Grace-1 na hivyo kupuuza mashinikizo na ombi rasmi la Marekani la kundelea kuishikilia meli hiyo. 

Akizungumza leo katika kikao cha wazi bungeni, Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa Waingereza wamejua kwamba hali ya mambo hii leo duniani si kama ilivyokuwa huko nyuma na wamelazimika kuacha uharamia baharini. 

Larijani ameashiria pia vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na kuwahutubu maafisa wa White House kwamba: Iwapo mnadhani kwamba kufanya hivyo ni kudhihirisha nguvu na misuli, basi mnapasa kufahamu kuwa wananchi wote wa Iran wamesimama imara dhidi yenu. 

Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran 
 

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa viongozi wa Marekani kwa upande mmoja wanatoa pendekezo la kufanya mazungumzo na Iran na katika upande wa pili, wanamuwekea vikwazo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hii. Amesema, wananchi wa Marekani wametumbukia katika kinamasi cha upotoshaji wa viongozi wao ambao wanaishi katika njozi. Dakta Larijani  pia amepongeza maadhimisho ya ushindi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika vita vya siku 33 na kueleza kuwa: Muqawama umetoa pigo kali kwa Wazayuni na Marekani na kuzima njama zao kwa ushindi ilioupata katika vita hivyo.