Rais Rouhani asisitiza kuimarishwa zaidi uhusiano wa Iran na India
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58059-rais_rouhani_asisitiza_kuimarishwa_zaidi_uhusiano_wa_iran_na_india
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kustawishwa na kuimarishwa zaidi uhusiano wa taifa hili na nchi ya India.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 23, 2019 09:44 UTC
  • Rais Rouhani asisitiza kuimarishwa zaidi uhusiano wa Iran na India

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kustawishwa na kuimarishwa zaidi uhusiano wa taifa hili na nchi ya India.

Rais Rouhani amesema hayo leo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India na kuongeza kuwa, kufanyika kikao cha kamisheni ya pamoja ya Tehran na New Delhi kunapelekea kupanuliwa ushirikiano wa pande zote baina ya nchi mbili hizi.

Rais Rouhani amesema kuwa, hakuna shaka kuwa, azma na irada imara ya Iran na India katika mustakabali itapelekea kustawishwa zaidi uhusiano na ushirikiano wa pande mbili.

Rais Hassan Rouhani akisalimiana na Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India

Rais Rouhani ameabinisha kwamba, kudhaminiwa na kulindwa usalama wa eneo kuna umuhimu mkubwa kwa Iran na India na kueleza kuwa, Tehran inafuatilia suala la kupunguzwa mizozo na mivutano na kupatikana usalama wa kudumu katika eneo hususan katika eneo la Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman.

Aidha amesema, ushirikiano wa pande kadhaa wa Iran na India na nchi nyingine ni muhimu na kusisitiza kwamba, Marekani haina budi kuondoa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran kwa haraka au kwa kuchelewa, kabla au baada ya uchaguzi wa Rais nchini humo.

Kwa upande wake, Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India sambamba na kusisitiza juu ya kupanuliwa ushirikiano katika sekta binafsi na za serikali za nchi mbili hizi amesema kuwa, Tehran na New Delhi zina uhusiano mzuri na mkongwe.