Meja Jenerali Salami: Marekani itajuta kutoa vitisho dhidi ya makamanda wa SEPAH
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58788-meja_jenerali_salami_marekani_itajuta_kutoa_vitisho_dhidi_ya_makamanda_wa_sepah
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Marekani inapaswa ichunge hatua inazochukua na akasisitiza kuwa: Wale ambao wametishia kuwaua kigaidi makamanda wa Iran, kama watabaki hai, bila shaka watajuta tu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2020 23:17 UTC
  • Meja Jenerali Salami: Marekani itajuta kutoa vitisho dhidi ya makamanda wa SEPAH

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Marekani inapaswa ichunge hatua inazochukua na akasisitiza kuwa: Wale ambao wametishia kuwaua kigaidi makamanda wa Iran, kama watabaki hai, bila shaka watajuta tu.

Meja Jenerali Hossein Salami ameyasema hayo leo kujibu vitisho vilivyotolewa na Marekani vya kuwaua shahidi makamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na akaongeza kwamba: Maadui wa Jamhuri ya Kiislamu wajue kuwa, kama wanawatishia kuwaua makamanda wa Iran, maisha ya yeyote kati ya makamanda wao hayatakuwa salama.

Meja Jenerali Salami amesisitiza kuwa: Ikiwa maadui watataka kuendeleza hatua zao haribifu, watakabiliwa na mazingira ambayo hawataweza kuyadhibiti.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, vitisho hivyo vinatokana na kushindwa Marekani dhidi ya Iran katika nyuga mbali mbali na akafafanua kuwa, wao wameshindwa katika nyuga za kijeshi na wamegonga mwamba pia katika uga wa vikwazo vyao vya kiuchumi.

Meja Jenerali Salami amesema, kuchukua hatua ya kuua kunadhihirisha dhati halisi ya utawala wa Marekani; na akakumbusha kwamba, wakati Marekani iliposhindwa kuizuia Iran isimiliki teknolojia ya kuitumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani iliamua kuwaua wanasayansi wa Iran, na baada ya kuona imeshindwa pia katika nyuga za kisiasa, kiuchumi, kisaikolojia na kijeshi imehisi haina njia nyingine ya kufanya isipokuwa kuua.

Kamanda mpya wa IRGC, Brigedia Jenerali Ismail Qaani

Amesema, kimsingi Marekani, utawala wa Kizayuni pamoja na tawala waitifaki wao na zilizo tegemezi kwao ni tawala za mauaji; na hivi sasa zimelazimika kuukiri rasmi na hadharani ukweli huo.

Ameongeza kuwa: Jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na kutishia kumuua pia kamanda mpya wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Brigedia Jenerali Ismail Qaani, vimedhihirisha ukweli muhimu kwamba, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ni tawala za mauaji.../